Wasifu wa Sera Lengwa

Author list: Shawn Dolley, Dan Hartman, Thea Norman and Ian Hudson

10th April 2021

Historia

Wakati mwingi, lengo la mwisho la utafiti wa kliniki ni mabadiliko ya sera, lakini mara nyingi kuna pengo kati ya utafiti na pande za sera inayoweza kusababisha kupotezwa kwa fedha na wakati. Kushughulikia haya, kifaa kipya kinachojulikana kama Wasifu wa Sera Lengwa (TPoP) kinaweza kutumika kabla ya kuanza kwa utafiti ili kutambua maswali muhimu ya utafiti, kusaidia maamuzi ya sera au kutumika wakati wa uzalishaji wa ushahidi na usambazaji wake. Wasifu wa Sera Lengwa linasaidia watafiti kuchambua ushahidi uliopo katika sera husika, pengo katika ushahidi huo na asili ya ushahidi utakikanao kujaza haya mapengo. Zaidi ya hayo, inawezesha mazungumzo ya mapema na ya kuendelea baina ya watafiti na wadau. Wakiwa wamejihami na maarifa haya pamoja na mahusiano haya, watafiti wa kliniki huongeza uwezekano waa masomo husika kukidhi mahitaji ili kutengeneza sera bora kwa njia inayofaa.